Deuteronomy 19

Miji Ya Makimbilio

(Hesabu 35:9-34; Yoshua 20:1-9)

1 aWakati Bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakapokuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao, 2 bndipo mtenge miji mitatu iliyopo katikati ya nchi kwa ajili yenu, katika nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa kuimiliki. 3Jengeni barabara katika miji hiyo na kuigawa mara tatu, nchi anayowapa Bwana Mwenyezi Mungu wenu kama urithi, ili kwamba yeyote amuuaye mtu aweze kukimbilia humo.

4Hii ndiyo kanuni kuhusu mtu amuuaye mwingine na kukimbilia humo kuokoa maisha yake, yaani, yeye amuuaye jirani yake bila kukusudia, wala hakumchukia kabla ya hapo. 5Kwa mfano, mtu aweza kwenda msituni na jirani yake kukata miti, naye anapozungusha shoka kuangusha mti, shoka linaweza kuchomoka kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake na kumuua. Yule mtu anaweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake. 6 cKama sivyo, mlipiza kisasi cha damu anaweza kumfuatilia kwa hasira kali, naye akamkamata na kumuua kama umbali ni mrefu sana hata ingawa hastahili kifo, kwa sababu amemuua jirani yake bila kukusudia. 7Hii ndiyo sababu nimewaagiza ninyi kutenga miji mitatu ya makimbilio kwa ajili yenu.

8 dKama Bwana Mwenyezi Mungu wenu akipanua nchi yenu, kama alivyoahidi kwa kiapo kwa baba zenu na kuwapa nchi yote aliyowaahidi, 9 ekwa sababu mmefuata kwa uangalifu sheria zote ninazowaamuru leo, kumpenda Bwana Mwenyezi Mungu wenu na kuenenda siku zote katika njia zake, ndipo mtenge miji mingine, mitatu zaidi. 10 fFanyeni hivi ili damu isiyo na hatia isimwagwe katika nchi yenu, ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa kama urithi wenu, ili kwamba msije mkawa na hatia ya kumwaga damu.

11 gLakini kama mtu anamchukia ndugu yake, akamvizia, akamshambulia na kumuua, kisha akakimbilia katika mmojawapo ya miji hii, 12wazee wa mji wake watatuma ujumbe kwake, kumleta kutoka mji ule na kumkabidhi mlipiza kisasi cha damu kumuua. 13 hMsimwonee huruma. Lazima mwondoe katika Israeli hatia ya umwagaji damu isiyo na hatia ili kwamba mpate kufanikiwa.

14 iUsisogeze jiwe la mpaka wa jirani yako ambao uliwekwa na wale waliokutangulia katika urithi upokeao katika nchi Bwana Mwenyezi Mungu wako anayowapa kuimiliki.

Mashahidi

15 jShahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lolote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lolote lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.

16 kKama shahidi mwenye nia ya kumdhuru mwingine akisimama kumshtaki mtu kwa uhalifu, 17 lwatu wawili wanaohusika katika mabishano lazima wasimame mbele za Bwana na mbele ya makuhani na waamuzi ambao wako kazini wakati huo. 18 mWaamuzi lazima wafanye uchunguzi kwa makini na shahidi akionekana kuwa ni mwongo, akitoa ushuhuda wa uongo dhidi ya ndugu yake, 19 nbasi mtende kama alivyotaka kumtendea ndugu yake. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu. 20 oWatu watakaosalia watasikia hili na kuogopa, uovu kama huo kamwe hautatendeka tena miongoni mwenu. 21 pMsionyeshe huruma, uhai kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.
Copyright information for SwhKC